ALICHOSEMA JAY Z KUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA KURUHUSIWA MAREKANI.

Beyonce na Jay Z kwenye Ikulu ya Marekani kumtembelea Obama
Rapper Jay Z amejitokeza hadharani na kuwa wa kwanza kuunga mkono kauli iliyotolewa na rais Barack Obama wa Marekani kuhusu kusupport ndoa za jinsia moja. Akiamplfy na CNN, Jigga amesema suala la kutoruhusu ndoa za jinsia moja kwa siku nyingi limekua likikwamisha taifa hilo kubwa duniani. Amesema hizo ishu ni ishu ambazo watu wanafanya vyumbani ndio maana haitakiwi kuwa ishu kubwa, kutowaruhusu watu kuwa na ndoa za jinsia moja ni sawa na kitendo cha kumbagua mtu kutokana na ngozi yake. Mwandishi wa habari wa CNN alipomwambia Jay Z kwamba haoni hiyo ishu inaweza kumuweka pabaya rais Obama ambae anategemea kura za wananchi kwenye uchaguzi mkuu ujao, Jigga alijibu “kura sio ishu, hii ishu ni kuhusu watu”

1 comment:

  1. jay z anajulikana ni freemason. Na sera za freemason ni kusapot mambo ambayo ni kinyume na neno la Mungu na kinyume na maadili ya kibinadam kwahiyo sishangai akisupport hilo. GOD FORBID

    ReplyDelete