Mwigizaji Wema Sepetu bado anaendelea kuishoot movie yake ya kwanza
iitwayo SUPER STAR ambayo inahusiana na maisha yake kwa asilimia kubwa
sana, ikiwa ni movie ambayo itaonyesha vitu vingi alivyovipitia kwenye
umaarufu wake.
Usiku wa May 29 kuamkia may 30 2012 saa nane na dakika kumi ndani ya
Maisha Club Dar es salaam, Wema alivishwa pete na mwimbaji Mwinyi wa
Machozi Band ambae kwenye hiyo movie yeye atazicheza nafasi zote za
Mwimbaji Diamond Platnums aliyewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na
Wema Sepetu, Mwinyi amecheza kama Diamond ambae pia alimvisha Wema pete
ya uchumba hapohapo Maisha Club.
Akiongea Exclusive na millardayo.com Wema amesema bajeti ya kutengeneza
hiyo movie ni kuanzia milioni 29 mpaka 30 ambapo alianza kuitengeneza
march mwaka huu na ataizindua june 23 2012.
Mrembo huyu ambae ni Miss Tanzania 2006 amesema mwanzoni alikua anataka
hii movie wacheze Irene Uwoya na Jb na ilikua haikua ikihusu maisha ya
Wema lakini baada ya Jb kuwa na kazi nyingi, alifikiria kucheza movie
mwenyewe na kupewa idea ya Super Star na msanii Suma Lee.
Alichofanya baada ya kupewa hiyo idea na Suma Lee ni kuipimp na kuongeza
matukio mengi aliyokutana nayo kwenye umaarufu na ni movie ambayo
mastaa wengi wa kibongo wameuza sura ndani yake.
No comments:
Post a Comment