Wema Sepetu’s Transformation!

Kadri muda unavyoyoma, tunazidi kuona Wema Sepetu akitokea kitofauti kimuonekano na hata kimavazi. na sasa,katika kile kinachosubiriwa kwa hamu,kuna ujio mpya wa Wema Sepetu,uliotangazwa na kampuni ya endless famme management. Ujio huo umezua gumzo ya aina yake kwenye anga za burudani huku wengi wakijiuliza kitakachojiri na nyota huyo wa filamu nchini. Kampuni hiyo ya Endless Fame Management,inayomilikiwa na Martin Kadinda,ambayo ndiyo inayosimamia shughuli za star huyo kwa sasa, imesema kwamba kuna shughuli nzito ambayo ameiandaa Wema, itakayowahusihsa mastaa wa muziki wa kike peke yake Bongo,pamoja na kumleta star mmoja muigizaji wa Nigeria, ambaye jina halijatajwa,ila kwa kugusia kampuni hiyo imetoa majina ya Omotola, Genevieve Nnaji au Rita Dominic wote wakiwa ni waigizaji nguli wa Nollywood.

No comments:

Post a Comment