Shilole Afunga Pub yake Kuheshimu Mwezi Mtukufu



WAKATI wengine wakiendelea kukomaa na kuunza vinywaji katika baa, zao msanii Zena Muhamed ‘Shilole’, amesema kuwa ameamua kuifunga Pub yake kwa lengo la kupisha mwezi mtukufu wa amadhani. Akiongea na mmoja wa waandishi wa mtandao wa DarTalk, aliyetembelea Pub hiyo na kukuta imefungwa, alidai kuwa yenye ni mtoto wa Kiisilamu hivyo hawezi kuacha sehemu hiyo iwe wazi wakati wateja wake wengi wamefunga. “Kwanza ni lazima niifunge kwa sababu mwezi huu ni kwa sisi waisilamu tunatakiwa kuachana na maovu yote ingawa watu huwa wanaacha kutenda maovu kwa kipindi hiki pekee,” alisema Shilole. Alidai kuwa anaamini kufunga kwake kutakuwa na manufaa makubwa kwani atakuwa anajipanga kwa ajili ya kufanya mambo makubwa zaidi baada ya kumaliza kwa mfungo.

No comments:

Post a Comment