KANUMBA KWELI ALIKUWA MTU WA WATU



Nimekuwepo msibani takribani masaa 8 nikiwa nimeambatana na viongozi wangu wa chama kuanzia diwani mwenyewe wa sinza
hakika watu ni wengi sana pale msibani....watu wa kila aina(matabaka yote) wamekuwa wakifika pale msibani kuhani wafiwa.
Nimependa namna mastaa wa sanaa mbalimbali wanavyojitolea kufanya kazi na kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri.
Mbali na msiba,Pia kuna mastaa walikuwepo pale msibani kwa namna moja au nyingine walikuwa ni gumzo kwa mfano Diamond Platnum alipowasili tu wananchi pale msibani walipiga kelele za kumshangilia...zaid ni pale alipokuwa anaondoka umati uliokuwepo nje ulilipuka kwa shangwe huku wapenzi wa jamaa huyu wakimsindikiza kwa namna ya maandamano hadi kwenye OPA yake.
Pia kundi la east coast team kwa mara ya kwanza wamekuja wakiwa pamoja pale msibani huku wakionesha ishara ya kuguswa sana na kifo cha The great..

Kanumba mungu alikupenda zaidi,,,REST IN PEACE

No comments:

Post a Comment