MDOGO WA KANUMBA AFUNGUKA,LULU AGOMA OYSTERBAY POLICE STATION

Ndugu wa Marehemu Steven Kanumba,Seth,ameelezea mkasa uliopelekea kifo cha kaka yake kilichotokea usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Sinza Vatican
Akielezea mbele ya waandishi wa habari Seth alisema kwamba Lulu alifika nyumbani kwa Kanumba usiku huo na baadae wakaanza kuzozana na Steven.Baada ya muda mfupi wote Kanumba na Lulu wakaingia chumbani..baada ya dakika chache Lulu alitoka chumbani na kuja kumuita Seth na kumwambia kuwa Steven kaanguka.Kusikia hivyo Seth aliingia chumbani haraka na kumkuta kaka yake amelala chini hajitambui.BNdipo alipochomoka mbio kwenda kumuita daktari wake Kanumba.Aliporejea hakumkuta Lulu
Dunia inataka kujua nini hasa kilitokea na masikio ya wengi yameelekezwa kwa Lulu ambaye kwa vyovyote vile anajua kilichotokea mule chumbani kwa kuwa yeye ndiye alikuwa na marehemu Kanumba chumbani kama wapenzi wakati balaa linapotokea.Lakini taarifa kutoka kituoni Oysterbay zinasema kwamba binti huyo mwenye umri wa miaka 18 amegoma kuongea chochote hadi awepo mwanasheria wake,na hata mwanasheria wake akifika ameomba arekodiwe kwenye kinasa sauti kila atakachoeleza kwa kuhofia ushahidi unaweza ukapindishwa baadae.Lulu bado yuko chini ya uangalizi mkali wa polisi
Mwanasheria mmoja ambae amejitambulisha kwa jina la Revocatus Alexandria Jr. ameomba wadau na waandishi kusubiri taarifa za kidaktari kuhusu chanzo cha kifo cha Kanumba.Amesema amekuwa akifuatilia sakata hili tangu lilipoanza na kwamba hakuna uthibitisho kuwa Lulu alimsukuma marehemu,inawezekana Kanumba mwenyewe katika vuta nikuvute alipoteza balansi na kudondoka bila ya kusukumwa.
Amefafanua zaidi kwa kusema hata kama Lulu alimsukuma marehemu sio lazima chanzo cha kifo kiwe ni kusukumwa.Jingine amesema inawezekana vile vile Kanumba alikuwa na tatizo la moyo au msukumo wa damu na hivyo alipokasirika msumo wa damu ulibadilika,au labda moyo uliashindwa kufanya kazi inavyotakiwa ndio maana alianguka
"Hata kama ni kweli alijigonga, subirini madaktari wathibitishe
chanzo cha kifo ndipo tuendelee kujadili!.
Najua msiba huu ni huzuni kubwa, lakini nawaombeni sana,
lets not be judgemental kwa Lulu!.
Mimi ni miongoni mwa waumini wakubwa wa the doctrine of
"karma", kuwa there is nothing new under the sun, hakuna coincidence wala bahati mbaya, lolote ambalo limetokea,
lilikuwa litokee tuu, yaani siku ya mpendwa wetu Kanumba
ndio ilikuwa imefika, saa ilipotimia Mungu akamuita, hata
asingesukumwa, angefia usingizini!.
Ni vizuri jamii tukafahamu si vema kuanza kuhukumu mtu kabla
ya preliminary investigation yoyote kufanyika

After all, there is life after life and life before life!, death ni
change tu ya life form from physical body to spiritual body!.

1 comment:

  1. R.I.P. SO SAD..BUT NI KWELI KABISA ..TUSUBIRI NA POLICE WASHAFANYA MAKOSA KUWARUHUSU WATU KUKUWEPO NYUMBANI POLE BILA UCHUNGUZI MAALAM KUFANYIKA...WASINGERUHUSU MTU YOYOTE KUFIKA KABLA YA WAO KUHAKIKISHA WAMEFANYA YOTE YANAYOTAKIKANA NA HASA KUJUA KINA NANI WALIKUWEPO MLE NDANI ..JAPO TWAAMBIWA NI KANUMBA,LULU NA MDOGO WAKE..ANYTHING CAN BE ON THAT NA KUFICHWA ...JE HUYO MDOGO WAKE ALIPOONDOKA KUMUITA DACTARI NA KURUDI NA KUMKUTA HUYU LULU HAYUPO..JE KULIKUWA NA MTU MWENGINE YOYOTE ALOFIKA PALE NYUMBANI ? NA JE ALOKUWEPO KWENYE SIM NA HUYU LULU NI NANI ? NA JE SIM HIYO POLISI WALIWEZA KUICHUKUA KWA UCHUNGUZI ? NA JE HUYU LULU WALICHUKUA MUDA GANI KUMFIKISHA KITUONI TO ARREST HER AND TOOK HER TO POLICE STATION ? NA ALIKUWEPO WAPI NA NANI.JE ALISEMA CHOCHOTE NA ALOKUWEPO NAO ? YANI JAMANI PENYE KIFO CHA GAFLA KAMA HICHI SIYO PAKUFANYIWA MCHEZO...HUYO LULU HATA AGOME VIP KUONGEA ATAONGEA TU NA WASIMUACHIE MPAKA ASEME WHAT HAPPEN ALL SHE GOT TO DO IS TELL THE TRUTH AND THE TRUTH IS WHAT WE ALL NEED TO KNOW" ABOUT STEVEN KANUMBA'S DEATH"

    ReplyDelete