Facebook Kuanza Kutengeneza Simu Kama iPhone!!



Theluthi ya watumiaji wa simu wako tayari kununua simu ya Facebook (smartphone) na asilimia 73 wanadhani wazo la mtandao huo kuwa na simu zake ni zuri.

Habari za simu hiyo zimeibuka wiki hii huku vyanzo vikidai kuwa Facebook imemwajiri engeener wa zamani wa Apple kutengeneza simu ‘rasmi’ ya Facebook.

Sio mara ya kwanza kwa simu za Facebook kuingia sokoni.

Mtandao huo wa kijamii uliwahi kuingia ubia na makampuni ya INQ na HTC kutengeneza simu za Facebook zikiwemo simu zilizowekewa button ya ‘Like’ ndani.

Simu hiyo inasemekana itakuwa tayari kuzinduliwa rasmi mwaka ujao.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na MyVoucherCodes kwa kuhoji watu 968, asilimia 32% wamesema watainunua ikiwa tayari.

Asilimia 57 wamesema wanaamini simu hizo zitakuwa na bei nafuu kuliko iPhone.

Baada ya iphone kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Samsung Galaxy, Facebook kuwa mpinzani mwingine mwenye nguvu? Yetu masikio.
Source

No comments:

Post a Comment