Mrembo mwenye tatizo la ngozi ageuka maarufu Mtandaoni Kwa make-up aliyobuni Mwenyewe
Msichana mwenye tatizo baya la ngozi liitwalo ACNE Cassandra Bankson amegeuka kuwa gumzo kwenye mtandao baada ya kujirekodi akijipiga make-up kutoa madoa madoa mengi mekundu aliyonayo.
Ang guess what! Unaweza kumsahau kwa namna alivyobadilika na kuwa na ngozi kama ya mtoto!
Video ya Cassandra, 19, kwenye YouTube imepata hits za kufa mtu ambapo anayoonesha namna ya kuficha tatizo lake kubwa la acne – lilisambaa usoni, shingoni, kufuani na mgongoni mwake.
Brunette huyu mrembo haswaaa ambaye kutokana na tatizo lake hilo alikuwa akizomewa na watu! Ametumia dakika kumi kufunika kabisa madoa hayo yenye muonekano mbaya kwa kutumia mbinu maalum ya make-up.
Na mwisho wa video hiyo Cassandra – anayejulikana kwa mashoga zake kama Cassy anaonekana kuwa na ngozi murua kama model aliye tayari kwa catwalk.
Tution aliyoitoa kupitia Youtube imeangaliwa mara milioni 7.5 huku watu wenye tatizo kama lake wakijifunza njia anayoitumia.
Cassy ambaye kwa sasa ni mwanamitindo, anasema zamani alikuwa anakataa kutoka nje ya nyumba yao kwasababu ya aibu ya kuwa na acne iliyopitiliza.
Ilibidi aache mpaka shule kwasababu ya kuzomewa na wanafunzi wengine.
Anasema: “Sikuwa naongea na marafiki na familia. Nilikuwa nafanya homework, nacheza na paka wangu na kujifunza jinsi ya kuweka make-up yangu.”
Kwa sasa Cassy anasema ujuzi wake wa make-up umemsaidia kutoka alikokuwa akijificha.
“Nililia kabla sijairekodi video na sikuipost mpaka miezi minne ilipopita sababu nilikuwa na wasiwasi namna gani watu watafikiria.”
Na baada ya kuipost video hiyo ilimchukua Cassy miezi mitano mingine kuangalia maoni ya watu.
“Nilidhani maoni yangekuwa mabaya kama yalivyokuwa ya shuleni, ” alisema.
“Lakini nilipoyasoma nilishangaa kuona watu walivyokuwa positive.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment