Russell Simmons: Beef ya Breezy na Drake imeisha
Nguli katika muziki wa hip hop nchini Marekani Russell Simmons ametangaza kuwa Chris Brown na Drake wamemaliza beef lao na hawana lengo la kuliendeleza.
Simmons ameongea na kambi zote mbili ili kuhakikisha kuwa drama hiyo haiwi kubwa kufuatia wasanii hao kupigana jumatano iliyopita na kuacha baadhi ya watu wakiwa na majeraha.
Wakati kuna ripoti kuwa rapper wa Young Money, Drake anaweza kukamatwa kwa kudaiwa kuanzisha fujo hiyo ya kurushiana chupa, Russell anasema issue hiyo sasa inaweza kumalizika.
“Nimeongea na pande zote za Chris Brown na Drake siku chache zilizopita kwa kuogopa kuwa tatizo linaweza kuwa kubwa. Sijauliza nini kilichotokea ama nani alianzisha, hiyo sio biashara yangu,” aliandika kwenye mtandao wake wa GlobalGrind.
“Pande zote mbili zimeniambia kuwa hazina mpango wa kuendelea na issue hii. Kwahiyo kwa wale wanaosubiri beef nyingine kubwa kama ya Biggie/Tupac, hakuna kitu kama hicho na bila shaka hakuna mtu anayeweza kujaribu kuingilia kutoka nje.”
“Watu wengi wanawaangalia Drake na Chris kwa ukaribu sasa hivi, wao wana uwezo wa kutoa ujumbe sahihi. Ninaheshimu sana usanii wa vijana hawa wote. Tuendelee kuwahimiza wafanye muziki mzuri unaoiburudisha dunia.”
Ugomvi huo unadaiwa kutokea kwa sababu ya Rihanna ambapo wote wamewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment